Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 06:34

Ukraine yasema Russia hairuhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia maelfu ya raia


Kikundi cha wakimbizi kituo cha duka la Tesco, kilichopo mpakani kati ya mji wa Medyka, na Przemysl, Poland, Ijumaa, Macih 4, 2022 kilichogeuzwa kuwa ni mahali pa Wakimbizi waliofanikiwa kuondoka Ukraine kupumzika. I (AP Photo/Marc Sanye)
Kikundi cha wakimbizi kituo cha duka la Tesco, kilichopo mpakani kati ya mji wa Medyka, na Przemysl, Poland, Ijumaa, Macih 4, 2022 kilichogeuzwa kuwa ni mahali pa Wakimbizi waliofanikiwa kuondoka Ukraine kupumzika. I (AP Photo/Marc Sanye)

Ukraine imesema Alhamisi Moscow imekataa kuruhusu huduma za kibinadamu kuokoa maelfu ya raia waliokwama katika maeneo yenye mashambulizi wakati pande zinazopingana zilishindwa kufanya chochote katika mazungumzo ya ngazi ya juu tangu Russia ilipoivamia Ukraine.

Vita vya Russia nchini Ukraine vinaingia wiki ya tatu huku kukiwa hakuna malengo yoyote yaliyofikiwa wakati ambapo maelfu ya raia wanauwawa, zaidi ya watu milioni mbili wamekuwa wakimbizi na maelfu wamekwama katika miji iliyozingirwa na mashambulizi huku mabomu yakiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amekutana na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov nchini Uturuki lakini amesema hakuna ahadi yoyote iliyotolewa na yeye kusitisha mashambulizi ili misaada iweze kuwafikia raia, ikiwemo Kyiv ambayo inahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kuondoa maelfu ya watu waliokwama katika eneo la bandari lililozingirwa la Mariupol.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati huo huo katika chumba tofauti, Lavrov hakuonyesha ishara zozote za maridhiano , akirudia madai ya Russia kwamba Ukraine kusalimisha silaha na kukubali hali ya kutoegemea upande wowote.

Amesema Kyiv ilionekana kutaka mikutano basi tu ili kuwepo mikutano na kwamba sitisho la mapigano halikutakiwa kuwa kwenye ajenda katika mazungumzo na Uturuki.

XS
SM
MD
LG