Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 21:33

Raia wa Ukraine wamekwama maeneo yaliyozingirwa na wanajeshi wa Russia

Wanajeshi wabeba majeneza wakati wa maziko ya Dmytro Kotenko, Vasyl Vyshyvany na Kyrylo Moroz, wanajeshi wa Ukraine waliouawa wakati wa uvamizi wa Russia nchini Ukraine, katika makaburi ya Lychakiv magharibi ya mji wa Lviv, March 9, 2022. Picha naYuriy Dyachyshyn / AFP)

Russia imetangaza sitisho jipya la mapigano Ukraine Jumatano, ili kuruhusu raia kuondoka katika miji iliyozingirwa.

Hata hivyo kulikuwa na ishara ndogo ya maendeleo yanayotoa njia za kuondoka kwa maelfu ya watu waliokwama bila dawa na maji safi ya kunywa.

Gavana wa mji wa Sumy ulioko mashariki amesema magari ya raia yalikuwa yanaondoka kwa siku ya pili kwa kutumia njia salama iliyotengenezwa kuelekea Poltawa upande wa magharibi.

Lakini majira ya mchana huko Ukraine hakukuwa na uthibitisho kwamba njia zote kwa ajili ya watu kuondoka zilifanikiwa kufunguliwa, ikiwemo njia kutokea Mariupol inayoonekana ni ya haraka zaidi, ambako shirika la msalaba mwekundu limeelezea kuwa hali huko ni mbaya sana .

Wasi wasi mkubwa wa kibinadamu ni Mariupol, bandari iliyoko kusini iliyozingirwa na wanajeshi wa Russia kwa zaidi ya wiki moja.

Wakazi wa huko wamekuwa wakijificha chini ya ardhi kutokana na mashambulizi ya mabomu, hawawezi kuwahamisha waliojeruhiwa na hawawezi kupata chakula , maji, umeme au joto.

XS
SM
MD
LG