“Tunapiga marufuku uagizaji wa mafuta yote na gesi kutoka Rashia, Biden amewambia waandishi wa habari kwenye Ikulu ya White House.
“Hiyo ina maana kwamba mafuta ya Rashia hatayakubaliwa tena katika bandari za Marekani”.
Rashia ni muazaji mkubwa wa mafuta na gesi ulimwenguni. Iliwekewa vikwazo vya kifedha duniani kutokana na vita vya Ukraine, lakini hadi sasa mauzo yake ya nishati yalikuwa yamesamehewa.