Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 08:14

Marekani inapiga marufuku uagizaji wa gesi na mafuta ya Russia


Bei ya gesi imepanda katika vituo vya mafuta Marekani
Bei ya gesi imepanda katika vituo vya mafuta Marekani

Marekani inapiga marufuku uagizaji wowote wa mafuta na gesi ya Russia, Rais Joe Biden alitangaza Jumanne hatua ambayo alisema italeta pigo jingine kubwa kwa mashine ya vita vya Putin, huku vikosi vya Russia chini ya uongozi wa Rais Vladmir Putin vikiendeleza mashambulizi yao dhidi ya Ukraine.

Hii ni hatua ambayo tunachukua ili kumuumiza zaidi Putin, Biden alisema. Lakini kutakuwa na gharama pia nchini Marekani. Bei ya gesi tayari imepanda hadi zaidi ya dola nne kwa galoni kiwango cha juu zaidi kuonekana nchini Marekani tangu mwaka 2008.

Msemaji wa White House, Jen Psaki alisema bei hizi za juu zinaweza kulaumiwa kwa mtu mmoja. Wamarekani wanalipa bei ya juu kwenye pampu kwa sababu ya hatua za Rais Putin, alisema. Huu ni msukumo wa Putin kwenye pampu ya gesi, ni mojawapo ya vichocheo vya vikwazo vyetu.

Lakini mbunge wa jimbo la California, m-Republican Kevin McCarthy alimkosoa Biden kwa kutohimiza uzalishaji zaidi wa mafuta Marekani.

XS
SM
MD
LG