Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 08:20

Rashia yaendelea kushambulia miji ya Ukraine, huku juhudi za kupokea wakimbizi zikiendelea.


Jengo lachomeka baada ya shambulio la kombora kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv. Machi 3, 2022. Picha ya AP
Jengo lachomeka baada ya shambulio la kombora kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv. Machi 3, 2022. Picha ya AP

Rashia hii leo imerudia tena mpango wake wa kufungua njia salama ili kuruhusu watu kukimbia kutoka miji inayozungukwa na wanajeshi wake na kukimbilia maeneo yenye usalama ndani ya Ukraine.

Hii ni baada ya Kyiv na washirika wake kukata hapo jana pendekezo la Moscow la kuwahamisha raia wa Ukraine hadi Rashia, wakisema ni njia ya kutafuta sifa na kuwatuhumu wanajeshi wa Rashia kutega mabomu ya ardhini na kushambulia kwa mizinga njia za kupita.

Hayo yakiarifiwa, ndege za kivita za Rashia ziliendelea kushambulia miji iliyo karibu na mji mkuu wa Kyiv, Kharkiv upande wa mashariki, Summy upande wa kaskazini mashariki na Mykolayiv kusini magharibi. Kulingana na maafisa wa serikali, watu 21 waliuawa wakati wa shambulio moja kwenye mji wa Summy Jumatatu usiku.

Na baada ya siku 13 za mapigano, Umoja wa mataifa unasema idadi ya wanaokimbia vita hivi sasa itafikia watu milioni 2 na kufanya hali hiyo kuwa mzozo mbaya kabisa wa wakimbizi kukimbia kwa wingi tangu vita vya pili vya dunia karibu miaka 80 iliyopita.

XS
SM
MD
LG