Bei ya bidhaa, ikiwemo ngano na mahindi, imeongezeka tangu Russia ilipoivamia Ukraine, Februari 24.
Russia na Ukraine ni wazalishaji wakubwa wa ngano na mahindi kote duniani.
Huku bandari za Ukraine zikiwa zimefungwa na Russia ikiwa imekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi, kuna wasiwasi kwamba kunaweza kutokea uhaba mkubwa wa nafaka hizo ambazo zinaagizwa na mataifa ya kigeni.
Afrika kusini, ambayo pia ni mzalishaji mkubwa wa mahindi, huagiza asilimia 40 ya ngano lakini mchumi mkuu katika taasisi ya kilimo na biashara Afrika kusini Wandike Sihlobo, amesema kwamba huenda uhaba mkubwa wa bidhaa hizo usitokee.