Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 03:27

Ukraine yafanikiwa kuzishambulia meli za kivita za Russia


Mwanajeshi wa Russia akilinda makao makuu ya meli za kivita za Russia katika Bahari ya Black Sea huko Sevastopol, Crimea, July 31, 2022.
Mwanajeshi wa Russia akilinda makao makuu ya meli za kivita za Russia katika Bahari ya Black Sea huko Sevastopol, Crimea, July 31, 2022.

Ukraine imetuma droni iliyokuwa na bomu ambayo imepiga  makao makuu ya meli za kivita za Russia katika Bahari ya Black Sea Jumapili.

Maafisa wanasema watu takriban watano walijeruhiwa katika shambulizii lililofanyika katika eneo la Sevastopol linaloshikiliwa na Russia.

Jumapili ni Siku ya Jeshi la Majini la Russia. Rais wa Russia Vladimir Putin aliadhimisha siku hiyo kwa kuhudhuria gwaride la maadhimisho Siku ya Jeshi la Majini huko St. Petersburg huku tangazo likitolewa kuwa jeshi la Majini la Russia limejiandaa kupokea kile alichokieleza kama makombora ya hypersonic Zircon katika miezi michache ijayo.

Silaha za Hypersonic huruka kwa spidi ya takriban Mach 5 na zina uwezo wa kubadili mwelekeo wakati zikiwa hewani. Ni tofauti na makombora ya balistiki, ambayo pia yanaweza kusafiri kwa spidi ya hypersonic ya takriban Mach 5 lakini yana mwelekeo ambao hauwezi kubadilika.

Uwezo wa kurusha silaha zinazoweza kubadilika kwa kiwango cha juu zikiwa na spidi ya hypersonic inaipa nchi fursa ya kutosha, kwa sababu aina ya silaha kama hizi zinaweza kupenya mfumo wa ulinzi wowote unaotumika hivi sasa.

“Haijalishi tishio hilo ni lipi. Iwapo huwezi kuliona, huwezi kujihami nalo,” Jenerali John Hyten, naibu mwenyekiti wa zamani wa Wakuu wa Pamoja wa Wafanyakazi, aliwaambia waliohudhuria Washington Januari 2020.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameiita Jumamosi kwa ajili ya watu kuondolewa kutoka jimbo la mashariki la Donetsk, mkoa ambao umeshuhudia mapigano makali wakati Russia ikitafuta udhibiti kamili.

Maelfu ya watu, wakiwemo watoto na watu wazee, wamebakia katika maeneo yenye vita katika mkoa mkubwa wa Donbas, ikiwemo Donetsk na Luhansk. Pia ni mkoa ambapo wafungwa wa kivita wa Ukraine walifariki baada ya shambulizi la kombora la kombora kutokea mapema wiki hii.

Zelenskyy alitoa tangazo hilo Jumamosi wakati akilihutubia taifa kwa njia ya video.

“Kadiri watu zaidi wanavyoondoka katika mkoa wa Donetsk hivi sasa, jeshi la Russia litapata fursa ya kuua watu wachache,” alisema, akiongeza kuwa wakazi walioondoka watalipwa fidia, alisema kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Zelenskyy aliahidi misaada wa kiufundi ili kuwashawishi watu waondoke.

“Wengi wamekataa kuondoka lakini hilo linahitaji kufanyika,” rais alisema. “Iwapo kuna fursa, tafadhali ongea na wale ambao bado wako katika maeneo yenye vita huko Donbas. Tafadhali washawishi kuwa ni muhimu waondoke.”

XS
SM
MD
LG