Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 01:02

Vikosi vya Russia vyatwaa mtambo wa pili kwa ukubwa wa umeme wa Ukraine

Vikosi vya Russia.
Vikosi vya Russia.

Afisa wa Ukraine alisema Jumatano kwamba vikosi vya Russia vimetwaa mtambo wa pili kwa ukubwa wa umeme wa Ukraine na wanafanya usambazaji tena mkubwa wa wanajeshi katika mikoa mitatu ya kusini mwa Ukraine.

Oleksiy Arestovych, mshauri wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, alithibitisha kutekwa kwa mtambo wa kufua umeme wa Vuhlehirsk katika eneo la mashariki la Donetsk. Lakini Arestovych alisema maendeleo hayo ni faida ndogo ya mbinu kwa Warussia.

Alisema upelekeaji tena wa majeshi ya Russia ulijumuisha kupeleka majeshi katika maeneo ya Melitopol, Zaporizhzhia na Kherson kama sehemu ya mabadiliko ya wazi katika juhudi ya mikakati ya kiulinzi .

XS
SM
MD
LG