Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 01:25

Macron aituhumu Russia kufanya ukoloni mamboleo


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akipigwa picha pamoja na Rais wa Benin Patrice Talon (kulia) kwenye ikulu mjini Cotonou, Julai 27, 2022. Picha ya AFP
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akipigwa picha pamoja na Rais wa Benin Patrice Talon (kulia) kwenye ikulu mjini Cotonou, Julai 27, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa ziarani nchini Benin Jumatano, ameitaja Russia kuwa “moja ya mataifa ambayo bado yanafanya ukoloni mamboleo” kufuatia uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

“Russia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine. Ni vita vya kudhibiti eneo, ambavyo tulidhani havipo tena kwenye ardhi ya Ulaya.”

“Ni vita vya kama vilivyofanyika katika karne ya 20, hata karne ya 19,” Macron amesema.

Ameongeza kuwa anazungumza akiwa katika bara ambalo lilitaabika kutokana na ukoloni mamboleo.

Akitoa matamshi hayo kwenye mkutano wa waandishi habari akiambatana na rais wa Benin Patrice Talon, Macron amesema “Russia ni moja ya mataifa ambayo bado yanafanya ukoloni mamboleo”, kwa sababu iliamua kuivamia nchi jirani ili kulinda maslahi yake.

Russia ilipeleka wanajeshi wake nchini Ukraine tarehe 24 Februari, na kuchochea vita ambavyo vimeua maelfu ya watu, na kuhamisha kwenye makazi yao mamilioni ya wengine na kusababisha wasiwasi wa mzozo wa kimataifa wa chakula kutokana na kuzuia usafirishaji wa nafaka ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG