Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 01:07

Russia yaushambulia mji mkuu wa Ukraine kwa makombora, watu 15 wajeruhiwa


Jeshi la Ukraine larusha makombora kuelekea upande wa wanajeshi wa Russia katika jimbo la Kharkiv, Julai 27, 2022. Picha ya AP
Jeshi la Ukraine larusha makombora kuelekea upande wa wanajeshi wa Russia katika jimbo la Kharkiv, Julai 27, 2022. Picha ya AP

Kwa mara ya kwanza katika wiki kadhaa, Russia Alhamisi imefanya mashambulizi ya makombora kwenye eneo la mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, na katika jimbo la kaskazini la Chernihiv, katika kile Ukraine inadai ni ulipizaji kisasi kwa kuwa inaendelea kusimama imara dhidi ya uvamizi wa Moscow.

Russia ilishambulia eneo la Kyiv na makombora sita ambayo yalirushwa kutoka bahari nyeusi, na kujeruhi watu 15, watano kati yao walikuwa raia, gavana wa jimbo la Ukraine amesema.

Ukraine inasema ilidungua moja ya makombora hayo lakini wanajeshi wa Russia walishambulia kambi ya kijeshi katika kijiji cha Liutizh nje ya mji mkuu, na kuteketeza jengo moja na kuharibu majengo mengine mawili.

Gavana wa jimbo la Kyiv Oleksiy Kuleba amehusisha mashambulizi hayo na maadhimisho ya siku ya uhuru ambayo Rais Volodymyr Zelensky alianzisha mwaka jana na ambayo Ukraine iliadhimisha jana Alhamisi kwa mara ya kwanza.

“Russia, kwa kutumia makombora, inazidi kulipiza kisasi kwa upinzani imara unaoungwa mkono na raia wengi, ambao Waukraine walifaulu kuupanga vizuri kwa ajili ya uhuru wao,” Kuleba ameiambia televisheni ya Ukraine.

“Ukraine tayari imekwamisha mipango ya Russia na itaendelea kujihami.”

Gavana wa jimbo la Chernihiv Vyacheslav Chaus ameripoti kwamba Russia ilifyatua pia makombora kutoka nchi jirani ya Belarus kwenye kijiji cha Honchariviska.

XS
SM
MD
LG