Majeshi ya Ukraine yametoa kanda zaidi za video siku ya Alhamisi ikiwa ni juhudi za kulitetea eneo lao kutokana na mashambulizi ya Russia. Swali ni iwapo vita vimefikia hatua ya kukwama lilitolewa na mshauri wa usalama wa taifa huko White House, Jake Sullivan wakati alipoonekana kwenye kituo cha televisheni cha ABC.
Sullivan, anasema “Unayaona majeshi ya Ukraine, kwa kweli yakipata mafanikio katika pande zote mashariki na kusini. Tumesema hapo kabla kuwa majibu ya mashambulizi haya yatakapoanza huenda yakawa magumu, na ymaekuwa magumu. Ndiyo hali ya vita, lakini waukraine wanaendelea kusonga mbele.”
Kama Sullivan alivyosisitiza kuwa utawala wa Biden una nia ya dhati kuipatia Ukraine silaha inazohitaji.
Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen, ambaye anaitembelea India, alizungumza kuhusu hatua nyingine ambazo zimechukuliwa kudhoofisha uchokozi wa Russia.
“Tutaendelea kuipunguzia fursa Russia kupata vifaa vya kijeshi na teknoloji ambazo inahitaji ili kupambana vita dhidi ya Ukraine. Moja ya malengo yetu makuu mwaka huu ni kupambana na juhudi za Russia kukwepa vikwazo,” amesema Waziri Yellen.
Wakati wa mkutano wa karibuni huko Vilnius, wanachama wa NATO walisimama pamoja na Kyiv, licha ya kutotoa mchakato wa wazi wa kujiunga na muungano huo.
Ian Brzezinski, Mchambuzi wa Sera za Mambo ya Nje, anasema, “tusidharau kile ambacho waukraine wamekipata katika hili. Kwanza, wamepata udhinishaji ulioendelea wa msaada kupita nia ya dhati ya kupatiwa msaada wa ulinzi wa muda mrefu, vifaa vya kijeshi na silaha.”
Lakini kwa uungaji mkono huo kuendelea kuwa kwenye nguvu wanachama wa NATO lazima waongeze michango yao ya kifedha, alisema seneta Mrepublican Dan Sullivan katika kipindi cha Meet the Press kwenye kituo cha televisheni cha NBC,
Seneta Mrepublican Dan Sullivan, ameelezea zaidi
“Ilidhoofisha uendelevu wa NATO, wakati ni mataifa saba tu kati ya 31 wanachama wa NATO ambao hivi sasa wanakidhibiti jukumu lao la asilia 2 ya GDP kwa ajili ya matumizi ya ulinzi. Liangalie hilo kwa maoni yangu lina dalili ya kudumaza hata uungaji kkono kwa Ukraine katika kipindi kifupi, na pia uungaji wa muda mrefu kwa NATO.”
Rais wa Marekani Joe Biden, hata hivyo, alielea bayana wiki iliyopita kwamba Ukraine haihitaji kusubiri kuwa mwanachama wa NATO ili kupatiwa uhakikisho wa ulinzi wa muda mrefu.
Alikuwa akizungumzia muundo mpya uliozindulwa na kundi la G7 mataifa yenye uchumi mkubwa ambao unafungua njia ya kuzungumzia mahitaji ya sasa ya Kyiv na ya baada ya vita.
Forum