Ratiba ya Biden inajumuisha kikao na rais wa Finland Sauli Niinisto kabla ya kukutana na viongozi wengine wakiwemo waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson, waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Store, waziri mkuu wa Denmrak Mette Frederiksen na waziri mkuu wa Iceland Kartin Jakobsdottir.
Kikao hicho cha Marekani na mataifa ya Scandinavia kinatarajiwa kuzungumzia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, ushirikiano wa usalama pamoja na teknolojia zinazoibuka. Finland na Sweden zilitoa ombi la kujiunga na NATO mwaka jana, baada ya Russia kuivamia Ukraine.
Finland na Sweden waliomba kujiunga na NATO ikiwa ni majibu ya uvamizi wa Russia huko Ukraine mwaka jana.
Muungano huo uliikaribisha Finland mwezi Aprili, lakini juhudi za Sweden zilichelewa baada ya Uturuki kulalamika kwamba Sweden imekuwa mpole sana kwa makundi ambayo Ankara yanayaona ni taasisi za kigaidi.
Forum