Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 04:07

Ukraine yadai kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Sudzha katika mkoa wa Kursk


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akiwa katika mazungumzo ya simu huko Kyiv. Picha na ofisi ya habari ya Rais wa Ukraine/ REUTERS.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akiwa katika mazungumzo ya simu huko Kyiv. Picha na ofisi ya habari ya Rais wa Ukraine/ REUTERS.

Rais wa Ukraine President Volodymyr amesema siku ya Alhamisi kuwa majeshi ya nchi yake yamechukua udhibiti kamili wa mji wa Russia wa Sudzha uliopo katika mkoa wa Kursk katika uvamizi wake katika ardhi ya Russia.

Mji huo, ulio mkubwa zaidi ambao Ukraine imeripotiwa kuuuteka mpaka sasa, kabla ya vita ulikuwa na wakazi takribani 5,000. Mji huo una kituo cha kupimia gesi ya asili ya Russia ambayo inapita kwenda kwenda kwenye mabomba ya Ukraine kuelekea Ulaya.

Wakati huo huo shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Kikosi maalumu cha Ukraine kilikamata kundi la zaidi ya wanajeshi wa Russia 100 siku ya Jumatano (Agosti 14) wakati wa uvamizi katika mpaka wa Kyiv, vyanzo vya usalama vya Ukraine (SBU) vimesema siku ya Alhamisi.

Reuters imeipata video iliyotoka kwa chanzo cha SBU ikionyesha kile ambacho chanzo hicho kinasema wanajeshi waliokuwa wamelala chini kifudifudi walikuwa wa Russia. Hakukuwa na uthibitisho wa tarehe au pahala iliporekodiwa video hiyo.

Wanajeshi 102 wa kikosi cha 488 cha Walinzi wa Russia wenye bunduki na kitengo chake cha "Akhmat", ndilo kundi kubwa zaidi la wanajeshi kukamatwa kwa wakati mmoja tangu Russia ilipoanzisha uvamizi wake kamili, chanzo hicho kimesema.

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika kifaru
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika kifaru

Mamlaka ya mkoa wa Kursk imeamuru watu kuhama katika eneo jingine ambalo limeathiriwa na mapigano baada ya majeshi ya Ukraine kuingia ndani wakiwa katika harakati za kuvuka mpaka katika mkoa wa Kursk.

Wizara ya Dharura ya Russia imetoa picha za video ikiwaonyesha watu wakipanda mabasi huko Rylsk na Lgovsk katika mkoa wa Kursk siku ya Jumatano.

Mamlaka za mkoa awali ziliamuru watu kuondoka katika maeneo kadhaa mengine.

Kaimu Gavana wa mkoa wa Kursk Alexei Smirnov amesema Jumatano usiku huduma za usalama, wanajeshi na mamlaka za ndani zitaratibu kuhama kwa wakazi kutoka katika eneo la Glushkovo kwenye mpaka na Ukraine.

Takriban watu 8,000 kutoka mkoa wa Kursk wamepatiwa hifadhi katika makazi ya muda kwenye mikoa kadhaa ya Russia, taarifa ya wizara hiyo imesema.

Kasi cha watu 121,000 wameondolewa Kursk au wamekimbia wenyewe maeneo yaliyoathiriwa na mapigano , maafisa wamesema.

Baadhi ya taarifa hii inatoka katika shirika la habari la AP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG