Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:21

Wanajeshi wa Chechenia wadaiwa Kuungana na Russia kukabiliana na Ukraine


Wanajeshi wa vikosi maalum vya Chechenia na wa vitengo vya kijeshi vilivyomo ndani ya vikosi vya ulinzi na usalama vya Russia. Januari 5, 2024. Picha na REUTERS/Chingis Kondarov
Wanajeshi wa vikosi maalum vya Chechenia na wa vitengo vya kijeshi vilivyomo ndani ya vikosi vya ulinzi na usalama vya Russia. Januari 5, 2024. Picha na REUTERS/Chingis Kondarov

Hii ni baada ya makabiliano na Waukraine katika eneo la Russia la Kursk.

Picha kama hizo za kamera zilizokuwa zimevaliwa mwilini zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya Telegram. Picha hii inaonyesha gari la jeshi lililowekwa alama ya pembetatu na miili kadhaa yenye sare za Ukraine wakati milio ya risasi ikisikika katika eneo hilo.

Shirika la habari la Reuters liliweza kuthibitisha eneo ambalo picha hizo zilipigwa. Tarehe haikuweze kuthibitishwa.

Siku ya Jumanne, vikosi yva Russia vilijibu mashambulizi yamajeshi ya Ukraine kwa makombora, droni na mashambulizi ya anga, ambayo kamanda mkuu mmoja amesema yameizuia Ukraine kusonga mbele baada ya shambulizi kubwa zaidi katika eneo huru la Russia tangu vita ianze.

Wiki iliyopita wanajeshi wa Russia waliharibu mpaka wa Russia katika shambulizi ya kushtukiza ambalo Rais wa Russia Vladimir Putin amesema lililenga koboresha nafasi ya Kyiv ya majadiliano kabla ya uwezekano wa mazungumzo kuanza na kupunguza kasi ya majeshi ya Russia kusonga mbele.

Forum

XS
SM
MD
LG