Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:52

Ukraine yaizamisha manowari ya Russia kwenye bahari Nyeusi


Manowari ya Russia iliyoripotiwa kuzamishwa na Ukraine katika bandari ya Sevastopol, Picha na Reuters
Manowari ya Russia iliyoripotiwa kuzamishwa na Ukraine katika bandari ya Sevastopol, Picha na Reuters

Jeshi la Ukraine limesema limeizamisha manowari huko Sevastopol inayodhibitiwa na Russia.

“Manowari ya Russia imezama chini ya bahari Nyeusi” amesema waziri wa ulinzi kupitia ukarasa wa X, akiitaja meli Rostov-on-Don ya kufanya shambulizi.

Afisa wa jeshi alisema shambulio kwenye bandari ya Sevastopol pia limesababisha uharibifu mkubwa kwa mitambo minne ya mfumo wa ulinzi wa S-400 "Triumf" ya kutungua ndege

Hakuna maoni ya haraka kutoka Russia kuhusiana na shambulio la Sevastopol.

Manowari ya dizeli ya umeme ya Rostov-on-Don iliongezwa kwenye jeshi la majini la Russia mwaka 2015.

Ilitengenezwa katika mji wa St.Petersburg nchini Russia imewekewa makombora ya Kalibr ambayo yanaweza kurushwa ikiwa chini ya maji.

Forum

XS
SM
MD
LG