Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:08

Zelenskyy asema Ukraine inahitaji silaha za masafa marefu kukabiliana na Russia


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy. Julai 15, 2024.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy. Julai 15, 2024.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy Jumapili amesema kuwa Ukraine inahitaji silaha za masafa marefu, ili kulinda miji pamoja na wanajeshi wake dhidi ya droni na makombora ya Russia.

Russia imefanya shambulizi la 5 la drone usiku kucha likiwa la karibu zaidi ndani ya muda wa wiki mbili zilizopita, lakini jeshi la Ukraine limesema kuwa liliharibu silaha zote za angani zilizorushwa. Jeshi la anga la Ukraine limesema kuwa silaha zilizorushwa zililenga maeneo 10 ya Ukraine.

Serhiy Popko ambaye ni mkuu wa jeshi la Kyiv amesema kuwa hakuna vifo au uharibifu ulioripoti mjini humo. “Usiku wa jana pekee, jeshi la Russia limerusha karibu makombora 40 aina Shahed, lakini karibu yote yameangushwa na walinzi wetu,” Zelenskyy amesema kupitia ujumbe wa Telegram. Ameongeza kusema kuwa kuna umuhimu wakuharibu ndege za kurusha mabomu kwenye viwanja vya ndege vya Russia, ili kulinda Ukraine dhidi ya mashambulizi.

“ Uwezo wetu wa kunasa silaha za masafa marefu ni jibu tosha kwa ugaidi wa Russia. Kila anayetusaidia, anasaidia kwenye vita dhidi ya ugaidi,” ameongeza Zelenskky. Zelenskyy Ijumaa akiwa mjini London ameendelea kutoa wito wake kwa washirika wa magharibi, kuruhusu utumizi wa silaha za masafa marefu, akiongeza kuwa Uingereza inahitaji kushawishi wenzake kuondoa kanuni zilizowekwa za kutotumia silaha hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG