Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:36

Ndege zisizo na rubani na makombora ya Russia zashambulia Ukraine na kuuwa raia wawili


Moshi unafuka kwenye eneo la shambulio la makombora ya Russia karibu na kituo cha treni cha Lukianivska huko Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Julai 8, 2024.
Moshi unafuka kwenye eneo la shambulio la makombora ya Russia karibu na kituo cha treni cha Lukianivska huko Kyiv, Ukraine, Jumatatu, Julai 8, 2024.

Ndege zisizo na rubani na makombora ya Russia yalipiga usiku kucha nchini Ukraine, na kuuwa raia wawili

Ndege zisizo na rubani na makombora ya Russia yalipiga usiku kucha nchini Ukraine, na kuuwa raia wawili na kugonga vituo vya nishati na miundombinu ya reli kote nchini, maafisa walisema Jumamosi.

Oleh Syniehubov, Gavana wa mkoa wa Kharkiv, alisema makombora ya Iskander yalilenga kituo cha miundombinu katika mji mdogo wa Barvinkove kaskazini mashariki, na kuuwa watu wawili na kujeruhi wengine watatu.

Hakutoa maelezo yoyote kuhusu kituo hicho, lakini alisema kwenye programu ya ujumbe wa Telegram kwamba zaidi ya nyumba 50 za makazi na majengo ya utawala na biashara pia yaliharibiwa katika shambulizi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG