Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:25

Zelenskiy anasema wanajeshi wa Ukraine wanazidi kusonga mbele ndani ya ardhi ya Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumatano alisema wanajeshi wa nchi yake “wanazidi kusonga mbele” ndani ya mkoa wa Russia wa Kursk na kudai kwamba mamia ya wanajeshi wa Russia walitekwa nyara au kujisalimisha.

Katika shambulizi kubwa kufanywa na jeshi la kigeni kwenye ardhi ya Russia tangu vita vya pili vya dunia, Kyiv ilisema inadhibiti maeneo 74 kusini magharibi mwa Russia.

Katika tukio tofauti, Ukraine ilishambulia usiku kucha viwanja vinne vya ndege vya Russia kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani katika “shambulizi kubwa” la aina yake tangu Moscow ilipoivamia Ukraine miaka miwili na nusu iliyopita.

Wakati Ukraine ikiukalia mkoa wa Kursk kwa wiki ya pili, Zelenskiy alisema kwenye mtandao wa kijamii, “Tunaendelea kusonga mbele. Kutoka kilomita moja hadi kilomita mbili katika maeneo tofauti tangu mwanzo wa siku.”

Viongozi wa Russia walikiri kusonga mbele kwa Ukraine katika mkoa huo lakini walisema walizima juhudi za wanajeshi wa Ukraine kutaka kusonga mbali zaidi ndani ya mkoa wa Kursk.

Forum

XS
SM
MD
LG