Hatua hii inafuatia marufuku ya usafiri iliyokuwa imeweka pamoja na nchi nyingine za Ulaya ili kudhibiti aina mpya ya Covid 19 kusambaa.
Wale wanaowasili Ufaransa lazima wawe wamepimwa na kuonekana hawana virusi vya corona na hilo liwe limefanyka chini ya saa 72.
Marufuku siyo tu imesitisha mtitiriko wa watu kote kwenye mipaka, lakini pia imesababisha kuvuruga kwa kiasi kikubwa cha usafirishaji bidhaa kati ya nchi hizo mbili.
Hatua hiyo imechochea khofu ya kutokea uhaba wa chakula na bidhaa nyingine.
Uingereza, Ufaransa na Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano Jumanne kufungua njia kwa marufuku hiyo kuondolewa.