Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:16

Mgogoro wa Uingereza kuondoka kabisa umoja wa ulaya unaendelea


Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson (kushoto) na mkuu rais wa halmashauri wa umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen (kulia)
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson (kushoto) na mkuu rais wa halmashauri wa umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen (kulia)

Uingereza imesisitiza kwamba umoja wa ulaya unastahili kubadilisha msimamo wake na kuruhusu kufanyika makubaliano ya kibiashara baada ya Uingereza kujiondoa umoja huo.

Lakini hatua hiyo imekosolewa na mkuu wa mazungumzo hayo, aliyetetea msimamo wa umoja huo akisema kwamba unastahili kulinda maslahi yake.

Mazungumzo yanatarajiwa kuendelea hii leo licha ya siku ya mwisho iliyowekwa na bunge la umoja wa ulaya kuwa jana jumapili.

Afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Uingereza ametaja mazungumzo hayo kuwa magumu kwa sababu ya tofauti kubwa zilizopo katika msimamo wa wahusika.

Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya Uingereza kuondoka rasmi kutoka umoja wa ulaya, pande zote zinataka kila mmoja kuchukua hatua na kuhakikisha kwamba mkataba unapatikana na kulinda biashara.

Kufikia sasa, hakuna hatua muhimu zimepigwa kufikia makubaliano yanayotafutwa.

Maswala yenye utata katika mazungumzo hayo ni kuhusiana na haki ya kuvua samaki katika maji ya Uingereza na kuweka viwango sawa vya shughuli za kibiashara kwa pande zote.

Uingereza ilijiondoa umoja wa ulaya Januari 31 na imekuwa katika mchakato wa kujiondoa kabisa tangu wakati huo. Inahitajika iwe imejiondoa kabisa kutoka soko la Pamoja na umoja wa forodha ifikapo mwishoni mwa mwaka.

XS
SM
MD
LG