Uingereza inakuwa taifa la kwanza la Magharibi kuwa tayari kuitoa kwa umma, ili kuzuia ugonjwa ambao umeathiri watu milioni 64 duniani ikijumuisha zaidi ya vifo milioni 1.4.
Mamlaka ya serikali ya kusimamia dawa, na bidhaa za afya imetoa ruhusa hiyo Jumatano kwa ajili ya chanjo hiyo kutumika.
Kampuni ya Pfizer ilitengeneza chanjo hiyo pamoja na kampuni ya Ujerumani ya BioNTech.
Chanjo ya kwanza itaanza kutolewa wiki ijayo kwa wafanyakazi wa huduma za afya wa Uingereza, kwa wazee wanaoishi katika vituo, na wafanyakazi wake watapewa kipaumbele maalumu.
Uingereza ni mongoni mwa nchi za ulaya zilizokumbwa vibaya sana na maambukizo vya virusi hivyo vinavyo weza kusababisha kifo ambapo karibu kesi milioni 1.6 za corona zimerekodiwa tangu janga hilo lilipozuka mwishoni mwa mwaka 2019.
Zaidi ya watu 59,000 wamekufa na corona hiyo ni kwa mujibu wa taarifa rasmi. Kampuni ya Pfizer imesema uamuzi wa Uingereza kuidhinisha kwa dharura chanjo hiyo ni hatua ya kihistoria wakati huu wa kupambana na janga la COVID-19.
Waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock Jumatano aliwashukuru wanasayansi kutoka kampuni ya Pfizer na BioNTech baada ya kuidhinisha chanjo yao ya COVID-19 kwa dharura.