Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:57

Uingereza kuanza kutoa chanjo dhidi ya Corona kwa raia wake kuanzia Jumatatu


Serikali ya Uingereza imesema kwamba inapanga kuanza kutoa chanjo ya Pfizer – BioNTech kwa watu nchini humo kuanzia jumatatu wiki ijayo.

Inakuwa nchi ya kwanza kuidhinisha chanjo dhidi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa majaribio makubwa.

Serikali ya Uingereza iliidhinisha matumizi ya chanjo hiyo jumatano wiki hii baada ya idhara ya kusimamia dawa na vifaa vya matibabu kutangaza kwamba chanjo hiyo ni salama kabisa kwa matumizi.

Hatua hiyo ni ufanisi mkubwa katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona, japo bado kuna changamoto namna chanjo hiyo itakavyotolewa katika nchi zenye mifumo mibovu ya afya.

Utafiti unaonyesha kwamba chanjo hiyo ina ufanisi wa asilimia 95.

Kampuni ya Pfizer inatarajia kupeleka dozi 800,000 nchini Uingereza katika siku chache zijazo.

Serikali ya Uingereza imesema kwamba imeagiza dozi milioni 40 ambazo zinatosha watu milioni 20,

Wafanyakazi katika makao ya watu wazee, madaktari na maafisa wengine wa afya watakuwa wa kwanza kupokea chanjo hiyo.

Watafuatiwa na watu wazee na watu wenye matatizo mbali mbali ya kiafya.

XS
SM
MD
LG