Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:53

Utafiti waonyesha aina mpya ya COVID-19 inakasi ya maambukizo zaidi

Wasafiri wakiweka alama katika mizigo kabla ya kuiwasilisha katika dawati la shirika la ndege la Uingereza British Airways, wakati serikali ya Mexico ikitafakari kusitisha safari za ndege kutoka Uingereza kutokana na hofu ya wimbi la aina mpya ya virusi vya corona.

Watafiti nchini Uingereza wanasema aina mpya ya COVID-19 ina maambukizo makubwa zaidi kuliko vya kwanza na huenda ikawa na maambukizi zaidi kwa watoto.

Wanasayansi katika taasisi ya New and Emerging Respiratory Virus Threats Advisory NERVTAG wamewaambia wana habari mapema wiki hii kuwa aina mpya ya kirusi kina kiasi cha asilimia 71 kuwa na maambukizi kuliko kile cha kwanza.

Aina mpya kutokana na virusi vya corona imelikumba eneo la kusini mwa Uingereza katika wiki za karibuni, na kuchochea nchi zaidi ya 40 kupiga marufuku ya usafiri kwenda na kutoka Uingereza.

Singapore, Ufilipino na Korea Kusini nao wameongezeka katika orodha hiyo ya Jumanne. Singapore imeweka marufuku isiyokuwa na muda maalum kwa abiria wote kutoka Uingereza.

XS
SM
MD
LG