Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:54

Waziri mkuu wa Eswatini afariki dunia


Waziri mkuu wa Eswatini Ambrose Dlamini wakati wa uhai wake akizugumza katika wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa COP 24 huko Katowice, Poland, Dec. 3, 2018.
Waziri mkuu wa Eswatini Ambrose Dlamini wakati wa uhai wake akizugumza katika wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa COP 24 huko Katowice, Poland, Dec. 3, 2018.

Waziri mkuu wa Eswatini, utawala wa mwisho kabisa wa kifalme wa Afrika, alifariki dunia katika hospitali moja ya Afrika Kusini Jumapili baada ya kuambukizwa virusi vya na corona, serikali ilisema katika taarifa.

Ambrose Dlamini, 52, alikuwa amelazwa katika nchi jirani ya Afrika Kusini mwanzoni mwa Desemba, wiki mbili baada ya kupimwa na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19.

"Wakuu wameamuru kwamba nijulishe taifa juu ya kifo cha kusikitisha na cha mapema cha Mheshimiwa Waziri Mkuu Ambrose Mandvulo Dlamini," Naibu Waziri Mkuu Themba Masuku alisema.

Waziri mkuu "alifariki mchana huu akiwa chini ya uangalizi wa matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini," akaongeza, bila kuelezea sababu ya kifo cha Dlamini.

Dlamini alikuwa ametangaza katikati ya Novemba kwamba alikuwa amekutwa na virusi vya corona lakini akasema kwamba alijisikia vizuri na alikuwa hana dalili.

Imetayarishwa na Sunday Shomari VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG