Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:49

UAE na Qatar zarejesha uhusiano wa kidiplomasia


Ubalozi wa Qatar nchini UAE.
Ubalozi wa Qatar nchini UAE.

Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar wametangaza kufunguliwa tena kwa balozi zao Jumatatu baada ya mvutano wa mwaka mzima.

Nchi hizo mbili zilitoa taarifa zikisema Ubalozi wa Qatar huko Abu Dhabi na Ubalozi mdogo wa Qatar huko Dubai, na pia Ubalozi wa UAE huko mji mkuu wa Qatar, Doha, ulikuwa umeanzisha shughuli zake tena.

Taarifa hizo hazikueleza iwapo mabalozi walikuwa tayari wamewasili au iwapo balozi hizo zilikuwa zimeanza kutoa huduma kwa umma.

Mawaziri wa mambao ya nje wa mataifa hayo mawili walizungumza kwa njia ya simu kupongezana kwa kufungua tena shughuli za kidiplomasia, Qatar ilieleza.

UAE iliungana na Saudi Arabia, Bahrain na Misri kuisusia na kuizuia Qatar mwaka 2017, sehemu kubwa kutokana na kufungamana na kuunga mkono vikundi vya Kiislam vyenye msimamo mkali kote Mashariki ya Kati ambavyo vilipata nguvu baada ya maandamano ya Mapinduzi ya Kiarabu (Arab Spring) mwaka 2011.

Nchi nyingine za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi wanaviona vikundi hivi kama magaidi – ikiwemo kikundi cha Muslim Brotherhood cha Misri, ambacho kilishinda uchaguzi huru na wa haki lakini kiliondolewa mamlakani baada ya mwaka mmoja wa utawala wake.

Qatar, kama zilivyo nchi nyingine za Kiarabu ni mshirika wa karibu wa Marekani, imekanusha mara kadhaa kusaidia vikundi vya kigaidi. Pia imewahi kuwa msuluhishi mkuu katika mashauriano ya vikundi vya wanamgambo wa Palestina na Hamas na Taliban ya Afghanistan yaliyoandaliwa na Marekani.

Mgogoro huo wa kidiplomasia ambao haujawahi kutokea kati ya marafiki wa nchi za Ghuba ya Kiarabu uliibua hofu ya kuzuka mgogoro wa kivita.

Lakini utajiri wa mafuta wa Qatar – na uhusiano wake wa karibu na Uturuki na Iran – kwa kiwango kikubwa uliiokoa kutokana na vikwazo vya kiuchumi na mahusiano polepole kurejea.

Kususiwa huko kulisitishwa rasmi mwezi Januari 2021. Mwishoni mwa mwaka jana, Qatar iliwakaribisha viongozi kutoka Saudi Arabia, Misri na UAE wakati ilipokuwa mwenyeji wa michezo ya Kombe la Dunia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG