Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:50

Antonio Guterres anatoa wito kwa Taliban kuondoa vikwazo dhidi ya wanawake Afghanistan


Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guterres

Mkutano huo wa siku mbili wa faragha katika mji mkuu wa Qatar, Doha, utajadili njia ya pamoja kusonga mbele jinsi ya kushirikiana na Taliban baada ya amri yao ya hivi karibuni ya kupiga marufuku wanawake wa Afghanistan kufanya kazi na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine yanayotoa misaada

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerudia kutoa wito kwa Taliban nchini Afghanistan kuondoa vikwazo dhidi ya haki za wanawake kufanya kazi na kupata elimu wakati akijiandaa kuitisha mkutano wa mabalozi kutoka nchi kadhaa Jumatatu kujadili hali katika taifa hilo linalokumbwa na mzozo.

Mkutano huo wa siku mbili wa faragha katika mji mkuu wa Qatar, Doha, utajadili njia ya pamoja kusonga mbele juu ya jinsi ya kushirikiana na Taliban baada ya amri yao ya hivi karibuni ya kupiga marufuku wanawake wa Afghanistan kufanya kazi na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine yanayotoa misaada.

Kutathmini hatua zote ambazo zinazuia haki za wanawake kufanya kazi ni muhimu kwa kuwafikia mamilioni ya watu nchini Afghanistan ambao wanahitaji msaada wa kibinadamu, Guterres aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumamosi jioni.

Wa-Afghanistan wanahitaji msaada wa dharura wa haraka. Wanawake ni muhimu ili kuhakikisha wanapata misaada alisema. Alisisitiza kuwa misaada ya kibinadamu ya wanawake inaleta huduma za kuokoa maisha kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema kizuizi dhidi ya wafanyakazi wa kutoa misaada kimeleta pigo kwa operesheni za kibinadamu nchini humo mahala ambako mamilioni ya Wa-afghanistan wanakabiliwa na njaa.

XS
SM
MD
LG