Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:43

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu wakutana Saudia kumaliza mzozo wa Syria


Waziri wa mambo ya nje wa Saudia Prince Faisal bin Farhan bin Abdullah amekutana na mwenzake wa Syria, Faisal Mekdad mjini Jeddah, Saudi Arabia, April 12, 2023. Saudi Press Agency/Handout via REUTERS
Waziri wa mambo ya nje wa Saudia Prince Faisal bin Farhan bin Abdullah amekutana na mwenzake wa Syria, Faisal Mekdad mjini Jeddah, Saudi Arabia, April 12, 2023. Saudi Press Agency/Handout via REUTERS

Mazungumzo miongoni mwa wanadiplomasia hao huenda sio rahisi kwani baadhi ya wanadiplomasia hao wanashikilia kwamba kurejesha uhusiano na Syria haiwezekani kwa sababu msingi wa Syria kuondolewa katika kundi la mataifa ya Kiarabu bado ni ule ule

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu wamekutana nchini Saudi Arabia kutafuta suluhisho la kumaliza vita vya Syria na kujadili namna ya kumaliza kutengwa kwa Syria na nchi za Kiarabu.

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka nchi sita za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ambazo ni Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Misri, Iraq na Jordan wako Saudi Arabia kwa ombi la ufalme huo.

Mazungumzo miongoni mwa wanadiplomasia hao huenda sio rahisi kwani baadhi ya wanadiplomasia hao wanashikilia kwamba kurejesha uhusiano na Syria haiwezekani kwa sababu msingi wa Syria kuondolewa katika kundi la mataifa ya Kiarabu bado ni ule ule.

Vita vya miaka kumi vya rais wa Syria, Bashar al-Assad vimesababisha vifo vya zaidi ya watu nusu milioni, na nusu ya idadi ya watu nchini humo wamelazimika kuyakimbia makaazi yao katika msako wa kikatili uliofuatiwa na maandamano. Hata hivyo baadhi ya viongozi wameanza kulegeza msimamo wao dhidi ya Assad baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyozikumba Syria na Uturuki hivi karibuni.

Jumamosi wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia ilisisitiza umuhimu wa kuwa na jukumu la uongozi wa nchi za Kiarabu katika juhudi za kumaliza mzozo huo.

XS
SM
MD
LG