Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:55
VOA Direct Packages

Rusesabagina awasili Qatar baada ya kuachiliwa na Rwanda kutoka jela


Rais wa zamani wa Marekani akiweka medali ya amani kwa Paul Rusesabagina. Picha ya maktaba.
Rais wa zamani wa Marekani akiweka medali ya amani kwa Paul Rusesabagina. Picha ya maktaba.

Msemaji wa serikali ya Rwanda amesema Jumanne kwamba nyota wa filamu ya Hotel Rwanda inayozungumzia mauwaji ya halaiki ya Rwanda ya 1994, Paul Rusesabagina amewasili Qatar baada ya kuachiliwa kutoka jela wiki iliyopita.

Rusesabagina ambaye ni mkazi wa Marekani alipewa kifungo cha miaka 25 jela Septemba 2021, kwa tuhuma za kuwa na ushirikiano na kundi linalompinga rais wa Rwanda Paul Kagame, na linalodaiwa kumiliki silaha. Rusesabagina aliachiliwa Ijumaa wiki iliyopita baada ya mashauriano ya miezi kadhaa kati ya serikali za Kigali na Washington.

Uhusiano wa karibu wa Kigali na Washington uliathirika kutokana na kufungwa kwa Rusasabagina pamoja na madai ya Marekani ambayo yamekanushwa na Kigali, kwamba Rwanda imetuma wanajeshi wake kwenye nchi jirani ya DRC, pia ikidaiwa kuunga mkono waasi.

Rwanda imesema kwamba kuachiliwa kwa Rusesabagina ni kutokana na dhamira ya kurejesha uhusiano mwema na Marekani. Rusesabagina mwenye umri wa miaka 68 aliwasili kwenye mji mkuu wa Qatar, Doha Jumatatu, kulingana na msemaji wa serikali Yolande Makolo.

XS
SM
MD
LG