Trump, ambaye ni Mrepublikan, alitaka katika pendekezo lake la bajeti mwaka 2019 kupunguza msaada kwa nchi nyingine lakini alikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka katika Bunge na ombi hilo halikufika mbali.
Bajeti yake ya hivi sasa anayopendekeza, ambayo itatolewa Jumatatu, ni muongozo wa pendekezo la matumizi ambalo siyo rahisi, kwa mara nyingine, kupitishwa, hususan katika mwaka huu wa uchaguzi.
Trump atataka kupunguza msaada kwa nchi nyingine kwa asilimia 21 katika pendekezo hilo, ambalo linataka dola bilioni 44.1 katika kipindi cha mwaka wa fedha unaokuja ukilinganisha na dola bilioni 55.7 zilizopitishwa katika mwaka wa fedha 2020, uongozi wa Trump umesema.
Msaada wa Ukraine utabakia katika kiwango kile kile cha 2020 katika pendekezo jipya. Trump alikutwa hana hatia wiki iliyopita kufuatia kesi iliyofunguliwa ikitaka kumuondoa madarakani kwa tuhuma za kuzuia msaada kwenda Ukraine akidaiwa kutaka Keiv imechunguze hasimu wake kisiasa Joe Biden, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratic na Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani.