Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:46

Marekani: Trump hana hatia, Seneti yatangaza


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump Jumatano alipatikana bila hatia katika kesi iliyomkabili ya kutaka kumwondoa mamlakani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka na kuzuia utendakazi wa Baraza la Wawakilishi la Marekani.

Kufuatia mchakato uliodumu kwa takriban miezi minne, na ulioigawanya Mareni kwa misingi ya kisiasa, mwendo wa saa Kumi na dakika 33 Jumatano alasiri, Jaji Mkuu wa Marekani John Roberts alitoa tamko kwamba kufuatia kura mbili zilizopigwa kwenye seneti siku hiyo, Rais Trump hakuwa na kesi ya kujibu.

Katika kura ya kwanza kuhusu tuhuma za utumizi mbaya wa mamlaka, maseneta 52 walimpata bila hatia huku 48 wakimpata na makosa.

Kwenye shtaka la pili la kuzuia kazi ya Baraza la Wawakilishi, maseneta 53 walimpata bila hatia dhidi ya maseneta 47.

Idadi ya maseneta iliyohitajika ili kummpata na hatia ni 67.

Katika kura ya kwanza, seneta Mrepublikan wa Jimbo la Uttah Mitt Romney amekuwa seneta wa kwanza katika historia ya Marekani, kupiga kura iliyokinzana na ya wenzake, akishirikiana na wademokrat katika suala lenye umuhimu mkubwa kama hilo.

Trump alikabiliwa na tuhuma za kukiuka katiba, kwa kushikilia msaada ya kifedha uliokuwa umeidhinishwa na bunge kuisaidia Ukraine kununua vifaa vya kijeshi vya kujikinga navyo.

Uamuzi wa Jumatano ulifuatia mchakato wa siku kadhaa ambap waendesha mashtaka wa chama cha Demokratik walitoa hoja zao kuwarai maseneta hao kumpata na hatia Rais Trump, wakifuatiwa na mawakili wa Trump ambao walijibu kwa kusema kuwa mteja wao hakuwa amafanya makosa yoyote.

Punde tu baada ya kupatikana bila hatia, Trump alituma ujumbe kupitia matandao wa Twitter, ambao ni wa video fupi inayoonyesa maandishi ya kuashiria kwamba ataendelea kuongoza kwa kipindi kirefu.

XS
SM
MD
LG