Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:44

Tanzania : Watu 14 wapoteza maisha katika mafuriko Tanga


Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tanga zimesababisha vifo vya watu 14, imeharibu miundo mbinu ya mawasiliano na kuharibu makazi ya watu katika mkoa huo. 

Watu 6 walipoteza maisha baada ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T890 CCX kutumbukia kwenye korongo baada ya daraja kubomoka kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Barabara iliyoharibiwa ni ya Handeni-Korogwe eneo la Sindeni, mkoani Tanga.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa mbali na kusababisha vifo mvua hiyo pia imesababisha watu kukosa makazi na wengine kukwama wakiwa safarini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Eneo hilo la barabara limekatika usiku wa kuamkia Jumapili na ajali imetokea alfajiri.

Taarifa zinasema idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua hizo tangu zilipoanza kunyesha imefikia 25.

Wilayani Korogwe kabla ya tukio hili walikufa watu 11 kati yao sita kwa kuangukiwa na nyumba na watoto watano kusombwa na mafuriko.

XS
SM
MD
LG