Mtalii mmoja bado hajulikani alipo na shughuli za kumtafuta zinaendelea, imesema mamlaka ya wanyama pori Kenya - KWS.
Watalii hao, raia 5 wa Kenya, mmoja wa kigeni na muongozaji wao walikumbwa na maji ya mvua walipokuwa wakiitembelea mbunga hiyo ya wanyama ya Hell’s gate.
Siku ya Jumapili, mbuga hiyo ilifungwa kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa watu hao walikuwa miongoni mwa kundi la watu 12 waliokuwa wanazuru hifadhi ya Hells Gate, karibu kilomita 100 Kaskazini magharibi mwa Jiji kuu la Nairobi.
Vyanzo vya habari Kenya vinaeleza manusra waliwajulisha maafisa wa hifadhi tukio hilo na juhudi za kuwatatufa watu hao zilianza.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.