Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:25

Shule zabadilishwa kuwa makazi au sehemu za biashara Kenya


Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Olympic Kibera, Nairobi, Kenya Jumatatu, Oct. 12, 2020.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Olympic Kibera, Nairobi, Kenya Jumatatu, Oct. 12, 2020.

Shule kadhaa za binafsi nchini Kenya zilifungwa wakati wa janga la COVID-19. Lakini baadhi ya shule zimebadilishwa malengo yake, ama zimekuwa ni makazi ya familia au, katika baadhi ya nyakati, zimekuwa ni sehemu ya biashara ya kuuza majeneza. 

John Kamand anauza majeneza kutoka kwenye eneo lake ambalo mpaka mwaka jana, lilikuwa na harakati nyingi.

Jengo ambalo lilikuwa likimilikiwa kwa ajili ya shule binafsi ya chekechea mjini Nairobi mpaka mwezi Julai, wakati janga la Covid 19 lilipolazimisha shule hiyo kufungwa..

“Janga la virusi vya corona ni moja ya mambo ambayo yametufanya kufungua duka hili, kwasababu shule imefungwa, na hakuna wanafunzi,” anasema Kamande.

Chama cha shule binafsi nchini Kenya kinasema karibu shule binafsi 400 zimelazimika kufungwa kwa sababu ya janga, na kuathiri takriban wanafunzi 56,000.

Hivi sasa majengo hayo yamefanyiwa mabadiliko, yamekuwa mduka, sehemu za kuhifadhi bidhaa na kwa matumizi mengine.

Watoto hivi sasa wanacheza kwa furaha katika uwa wa shule hizo—lakini hivi sasa hakuna shule.

Watoto hao wanaishi na familia zao katika kile kilichokuwa madarasa baada ya shule kugeuzwa na kuwa sehemu ya nyumba ya kupangisha.

Nassiri Kirui mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akifundisha hesabu na sayansi kabla ya shule kufungwa na kubaki kwenye eneo hilo la shule kama meneja wa jengo.

Kirui anasema “nilikuwa hapa kama mwalimu. Lakini kwasababu ya fedha, sina fedha, ndiyo maana nimekuwa muangalizi.”

Wakati shule za Kenya zilifunguliwa mwezi Januari mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu kufungwa mwezi Machi, matokeo ya kufungwa kwa shule binafsi huenda yatahisiwa kwa muda fulani ujao.

Mutheo Kasanga ni mwenyekiti wa taifa wa chama cha shule binafsi Kenya anasema, “tuna mwanya mkubwa sana katika nchi yetu, na jamii yetu inazidi kukua – katika hesabu ya mwisho ya idadi ya watu imeonyesha ongezeko la milioni moja. Kwahiyo tuna kazi nyingi za kufanya.”

Serikali ya Kenya mwezi Septemba iliahidi kiasi cha dola milioni 64 ikiwa ni msaada kwa shule binafsi lakini bado haijatekeleza hiyo ahadi yake.

XS
SM
MD
LG