Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:11

Serikali yaeleza waliouwa watu 100 Burkina Faso ni magaidi


Burkina Faso
Burkina Faso

Watu wenye silaha wamewaua raia wapatao 100 katika shambulio la usiku wa kuamkia Jumamosi, kwenye kijiji kimoja kaskazini mwa Burkina Faso, serikali imesema leo Jumamosi. 

Taarifa ya serikali inaeleza kwamba washambuliaji hao waliwaua wakazi wa kijiji cha Solhan, katika mkoa wa Yagha, kwenye mpaka wa nchi hiyo na Niger, kabla ya kuteketeza nyumba na soko, inaripoti Reuters.

Serikali iliwataja washambuliaji kama magaidi, lakini hakuna kundi lililodai kuhusika. Mashambulizi ya wanajihadi wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya al-Qaida, na Islamic State katika eneo la Sahel, Magharibi mwa Afrika, yameongezeka sana tangu kuanza kwa mwaka, haswa Burkina Faso, Mali na Niger, huku raia wakiwa waathirika wakuu.

Serikali ilitangaza kipindi cha saa 72 za maombolezo ya kitaifa na kusema kuwa idadi ya watu waliouawa ni takriban 100.

Vurugu nchini Burkina Faso zimepelekea zaidi ya watu milioni 1.14 kukimbia makwao, kwa zaidi ya miaka miwili, wakati nchi hiyo maskini, na inayokabiliwa na ukame, pia inawapa hifadhi wakimbizi wapatao 20,000 kutoka nchi jirani ya Mali, ambao wanatafuta usalama kutokana na mashambulio ya wanajihadi.

XS
SM
MD
LG