Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:56

Rwanda na DRC zaendelea kunyoosheana vidole, kila upande ukimtuhumu mwenzake


kushoto ni Rais wa DRC Felix Tshisekedi, na kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame
kushoto ni Rais wa DRC Felix Tshisekedi, na kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame

Mivutano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Kongo inapamba moto, baada ya Kigali kuishutumu Kinshasa kwa kuhujumu  jitihada za kikanda zinazoendelea za  kuleta amani mashariki mwa nchi hiyo.

Mivutano inaelekea kusambaa, Alhamisi baada ya Kigali kudai kwamba Kongo ilikuwa inajiandaa kwa vita kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni.

Rwanda inadai Kinshasa inaendelea kutoa silaha na majeshi yake yanapigana kwa kushirikiana na makundi haramu yenye silaha, mashariki mwa DRC, kikiwemo kikundi cha mauaji ya kimbari cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).

“Hii pia inaonyesha wazi ukiukaji wa makubaliano ya Nairobi yaliyokuwa na lengo la kuwanyang’anya na kuviondoa vikundi hivyo vyenye silaha, ambavyo ni tishio kwa usalama wa Rwanda,” ilisema taarifa iliyotolewa Alhamisi.

Taarifa hiyo imekuja saa chache baada ya rais wa Kongo Félix Tshisekedi kuwaambia viongozi wanaohudhuria mkutano unaoendelea wa Jukwaa la Kiuchumi la Kimataifa (WEF) huko Davos, Uswizi, kuwa Rwanda ni “ kizuizi cha maendeleo ya kikanda “na kwamba M23 hawajajiondoa katika maeneo waliyoyateka hivi karibuni licha ya kuwepo shinikizo la kimataifa.

Wanajifanya kuondoka, wanajifanya wanasogea, lakini sivyo. Kwa kifupi wanazunguka palepale, wanahamia sehemu nyingine, na wanaishi katika miji wanayoishikilia” Tshisekedi alisema katika jopo la mkutano wa WEF.

Kigali imedai maandamano yaliyofanyika dhidi ya uwepo wa majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) huko Goma na maeneo mengine ya DRC ni sehemu ya mpango wa jeshi la DRC na serikali wa kutaka kujitoa katika mchakato wa amani wa Nairobi na Luanda.

Na kuongeza kuwa lengo la maandamano hayo inaelekea yalikuwa na kusudio la kufanya majeshi hao yaondoke, wakati taarifa kutoka azimio la Luanda ni “kuendelea kikamilifu kupelekwa kwa majeshi ya EAC.

Chanzo cha habari hii kinatokana na gazeti la "The East Africa" linalochapishwa Kenya.

XS
SM
MD
LG