Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:29

Rwanda: DRC inajitayarisha kwa vita, imesajili mamluki


Waasi wa M23 wakipumzika, Karambi, mashariki mwa DRC,kivu kaskazini karibu na mpaka na Uganda, July 12, 2012.
Waasi wa M23 wakipumzika, Karambi, mashariki mwa DRC,kivu kaskazini karibu na mpaka na Uganda, July 12, 2012.

Serikali ya Rwanda imesema kwamba Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC inasajili mamluki na kuvuruga mchakato wa kuleta amani nchini humo.

Rwanda imedai kwamba DRC inajitayarisha kwa vita na haijatoa ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba DRC imesajili mamluki.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi amesema wiki hii akiwa Uswizi kwamba waasi wa M23 wamekataa kuheshimu mchakato wa amani na kwamba hawajaondoka katika sehemu walizokuwa wanashikilia licha ya kusema kwamba wameondoka.

Waziri wa mambo ya nje wa DRC Christophe Lutundula, amenukuliwa na vyombo vya habari vya DRC akisema kwamba waasi was M23 na serikali ya Rwanda wamekataa “kuheshimu makubaliano ya kurejesha amani.”

Lutundula amesema serikali ya Kinshasa “italinda mipaka yake” na kuonya kwmaba “kwa nguvu zote, tutalinda ardhi yetu.”

Maandamano yamekuwa yakifanyika mashariki mwa DRC katika mji wa Goma kulalamikia utendakazi wa jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki.

Waandamanaji wana mtazamo kwamba wanajeshi wa jumuiya hawafanyi kazi kwa haraka kuwaondoa waasi wa M23 sehemu hiyo.

Serikali ya Kigali imesema kwamba “Serikali ya Rwanda inasikitishwa na taarifa iliyotolewa na serikali ya DRC Januari 18, 2023, ambayo haijatilia maanani makubaliano ya Luanda Angola, ya Novemba 23, 2022.”

‘Maandamano ya kupangwa’

Rwanda imedai kwamba maandamano yanayoendelea mashariki mwa DRC yamepangwa, na kwamba ni sehemu ya mkakati wa DRC kujiondoa kwenye mchakato wa amani wa Luanda na Nairobi.

Waasi wa M23 wameondoka kutoka baadhi ya miji muhimu ambayo wamekuwa wakidhibithi, mashariki mwa DRC.

Idadi kubwa ya wakimbizi wanaendelea kuvuka mpaka na kuingia Rwanda kutokana na mapigano DRC.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alitishia kuwaondoa wakimbizi kutoka DR, lakini baadaye serikali yake ilidai kwamba alinukuliwa vibaya.

DRC inadai kwamba Rwanda inawasaidia waasi wa M23, madai ambayo vile vile yametolewa na mataifa ya magharibi pamoja na ripoti ya wataalam wa umoja wa mataifa. Rwanda imefutilia mbali madai hayo na badala yake inadai kwamba DRC inaunga mkono waasi wa FDLR ambao rais Paul Kagame amedai kwamba wana lengo la kupindua serikali yake.

XS
SM
MD
LG