Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:20

Waomba hifadhi Uingereza wakubaliwa kukata rufaa dhidi ya mpango wa kuwapeleka Rwanda


Mabango ya kupinga "uhamishaji haramu" wa binadamu.
Mabango ya kupinga "uhamishaji haramu" wa binadamu.

Mahakama Kuu ya Uingereza, Jumatatu ilitoa kibali kwa kundi la waomba hifadhi kukata rufaa, dhidi ya uamuzi kwamba mpango wa Uingereza kupeleka wahamiaji Rwanda ni halali.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza ilisema itatetea sera yake, ambayo ni sehemu kuu ya mpango wa Waziri Mkuu Rishi Sunak, kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili kwa boti ndogo.

Serikali inasema mpango huo utazuia usafirishaji haramu wa binadamu, ingawa umelaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu na hata Mfalme Charles tangu ulipotangazwa mwezi Aprili.

Safari ya kwanza ya ndege iliyopangwa kuwahamishia wahamiaji hao hadi Rwanda, ilizuiliwa mwezi Juni mwaka jana, baada ya uamuzi wa dakika za mwisho wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, ambayo iliweka amri ya kuzuia uhamishaji wowote hadi kukamilika kwa hatua za kisheria nchini Uingereza.

Mwezi uliopita, Mahakama Kuu iliamua kuwa ni halali kwa Uingereza kufanya mipango na serikali ya Rwanda kuwatuma waomba hifadhi huko, lakini ikakubali kusikilizwa kwa changamoto za kisheria zilizowasilishwa na watu wanane wanaotafuta hifadhi.

XS
SM
MD
LG