Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:54

Waasi wa M23 wanajiimarisha katika sehemu tofauti za DRC


Waasi wa kundi la M23 wakiondoka Rumangabo baada ya kuachilia mji huo kwa wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki Jan 6, 2023
Waasi wa kundi la M23 wakiondoka Rumangabo baada ya kuachilia mji huo kwa wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki Jan 6, 2023

Ripoti ya ujasusi ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba waasi wa M23 wameendelea kujiimarisha katika sehemu nyingine za mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kwamba wanaondoka katika miji ambayo wamekuwa wakiishikilia na kuikabidhi kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ripoti hiyo vile vile inasema kwamba waasi wa M23 wapo katika sehemu za Kibumba, Kivu kaskazini, ambako waliripotiwa kuondoka mwezi Desemba tarehe 23, na kwamba waasi hao wameimarisha shughuli zao katika sehemu nyingine na hivyo kupelekea kuwepo hali ya kutoeleweka kuhusu vita vya mashariki mwa DRC.

Kundi la waasi la M23, linalopigana na wanajeshi wa serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limekuwa likiondoka sehemu ambazo lilikuwa linadhibithi zikiwemo kambi za jeshi za serikali, mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini.

Waasi hao wameondoka mji wa Rumangabo, kilomita 40 kaskazini mwa mji wa Goma, na sehemu hiyo sasa inaongozwa na jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

DRC, mataifa ya Magharibi na Umoja wa Mataifa wanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Rwanda inakanusha.

DRC: Waasi wa M23 wamekubali kuondoka Rumangabo
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:30 0:00

XS
SM
MD
LG