Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:38

Wachambuzi wa masuala ya kisasusi kutoka UN watoa ripoti kuhusu waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo


Wapiganaji wenye silaha nchini kwenye picha ya maktaba.
Wapiganaji wenye silaha nchini kwenye picha ya maktaba.

Wachambuzi wa masuala ya kijasusi kutoka Umoja wa Mataifa wameshuhudia harakati zinazoshukiwa kufanywa na waasi wa M23 katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo kundi hilo lilibidi kuondoka.

Hayo ni kwa mujibu wa nyaraka za ndani za Umoja wa Mataifa, ambazo pia zinasema kuna dalili kwamba kundi hilo lenye silaha limeteka maeneo mengine. Matokeo hayo yanaashiria kuendelea kutokuwa na uhakika kuhusu hali halisi ya mzozo kati ya waasi na wanajeshi wa serikali katika jimbo Kivu Kaskazini.

Kundi la M23 lilihitajika kuondoka eneo la Kibumba kufikia Desemba 23, kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na viongozi wa Afrika Mashariki. Hata hivyo, ripoti ya siri kutoka Kituo cha Uchambuzi wa Misheni ya Pamoja ya kitengo cha ujasusi cha Umoja wa Mataifa ilisema "kujiondoa kabisa" "bado haijathibitishwa" na kwamba "harakati zinazoshukiwa za M23 bado zilionekana katika eneo hilo".

Ripoti hiyo inayoangazia kipindi hadi Januari 3 pia inaangazia mifano ya M23 kutwaa eneo jipya mahali tofauti. Takriban watu 450,000 walilazimika kuyakimbia makaazi yao mwaka jana katika mashambulizi mapya yaliyofanywa na kundi hilo la waasi linaloongozwa na Watutsi.

XS
SM
MD
LG