Rais Tshisekedi, amewashutumu wanamgambo hao kwa kudanganya makubaliano ya kuondoa vikosi vyake.
Viongozi wa kikanda walifikia makubaliano Novemba mwaka jana ambapo kundi hilo la Kitutsi lilipanga kujiondoa katika maeneo inayo shikilia ifikapo Januari 15.
Hiyo ilikuwa ni sehemu ya juhudi za kumaliza mgogoro ambao umewakosesha makazi watu 450,000 na kuzusha mgogoro wa kidiplomasia baina ya Congo na jirani yake Rwanda.
Akiwa Davos, Uswizi, katika mkutano wa ulimwengu wa uchumi rais Tshisekedi, alisema licha ya msukumo wa kimataifa kundi hilo bado lipo katika maeneo hayo.
Ameongeza kusema kundi hilo linajifanya kuondoka lakini ukweli ni kwamba bado lipo katika maeneo inayoshikilia.