Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:34

Russia yasema mifumo yake ya ulinzi wa anga imetungua droni za Ukraine zilizo shambulia Moscow


FILE PHOTO: Wanajeshi wa Ukraine wakishambulia majeshi ya Russia karibu na mkoa wa karibu wa Zaporizhzhia.
FILE PHOTO: Wanajeshi wa Ukraine wakishambulia majeshi ya Russia karibu na mkoa wa karibu wa Zaporizhzhia.

Russia imesema Jumanne mifumo yake ya ulinzi wa anga imezitungua ndege za Ukraine zisizo na rubani katika anga ya Moscow na eneo la Bryansk lililoko mpakani kati ya nchi hizo mbili.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema shambulizi katika eneo la Moscow lilihusisha droni mbili na hakuna uharibifu ulioripotiwa.

Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin, alisema katika ujumbe wa Telegram kuwa droni moja ilitunguliwa katika eneo la Krasnogorsk upande wa kaskazini magharibi mwa Moscow na nyingine huko eneo la Chastsy magharibi mwa mji huo.

Shirika la habari la Reuters lilisema kuwa kulikuwa na uharibifu mdogo katika jengo refu la makazi ya watu huko Krasnogorsk na vifuzi vilivyoanguka viliharibu magari yaliyokuwa chini.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema droni mbili za Ukraine zilitunguliwa na mifumo inayokinga shambulizi iliyoko katika anga ya Bryansk zilidondoka bila ya kusababisha vifo vyovyote.

Mashambulizi ya anga yanayofanywa na Ukraine yalisababisha viwanja vya ndege vya Moscow kusimamisha safari za ndege kwa kipindi fulani, hatua ambayo imechukuliwa ili kukabiliana na mashambulizi ya droni katika mji mkuu wa Russia katika siku zilizopita.

Russia pia ilisema ndege za kijeshi aina ya Sukhoi ziliiharibu boti ya uchunguzi ya Ukraine iliyokuwa katika eneo la mitambo ya kuzalisha gesi ya Russia katika bahari ya Black Sea.

Taarifa ya wizara ya ulinzi haikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo, ikiwemo sehemu hasa ambapo tukio hilo lilitokea.

Papa Francis akiwa na Jenerali wa Marekani Mark Milley, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi walipokutana Vatican, Agosti 21, 2023.
Papa Francis akiwa na Jenerali wa Marekani Mark Milley, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi walipokutana Vatican, Agosti 21, 2023.

Papa Francis na Jenerali wa Marekani Mark Milley, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi, walijadili suala la vita vya Ukraine huko Vatican Jumatatu.

Milley, ambaye ni Mkatoliki, alisema ziara yake ilikuwa na umuhimu mkubwa kwake, kulingana na msemaji wa Milley, Kanali Dave Butler.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG