Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:50

Uholanzi na Denmark zakubali kuipa Ukraine ndege za kivita kukabiliana na mashambulizi ya Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte wakitembea karibu na ndege aina ya F-16 mjini Eindhoven, Uholanzi, Agosti 20, 2023
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte wakitembea karibu na ndege aina ya F-16 mjini Eindhoven, Uholanzi, Agosti 20, 2023

Uholanzi na Denmark zimekubali kuipa Ukraine ndege za kivita aina ya F-16 ili kukabiliana na mashambulizi ya Russia.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alifanya ziara nchini Uholanzi Jumapili katika juhudi ya kushinikiza aendelee kupewa misaada ya kuimarisha mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine, baada ya Marekani kuridhia Denmark na Uholanzi zipeleke nchini Ukraine ndege za kivita aina ya F-16.

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte alimwambia Zelenskiy kwamba nchi yake na Denmark zitatoa ndege hizo kwa Ukraine, lakini amesisitiza kuwa ndege hizo zitatolewa mara tu baada ya masharti ambayo hakuyataja yatakuwa yametimizwa.

Uholanzi na Denmark katika miezi ya karibuni ziliongoza juhudi za kimataifa kuwapatia mafunzo marubani wa Ukraine kuendesha ndege hizo na hatimaye kuzikabidhi Ukraine ili kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia, iliyoivamia Ukraine tangu Februari 2022.

Zelenskiy alisema kwenye mtandao wa Telegram “ Suala kuu ni ndege za F-16 kwa Ukraine kulinda wananchi wetu dhidi ya vitisho vya Russia. Tunazidi kupata nguvu.”

Ziara hii inahusu pia mkutano wa kimataifa wa amani na kuifikisha Russia mbele ya vyombo vya sheria, Zelenskiy alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG