Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:11

Ukraine wasema Russia imeharibu miundo mbinu ya kuhifadhi nafaka katika bandari ya Odesa


Ghala iliyoharibiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Russia inaonekana kwenye bandari ya Danube karibu na Odessa, Ukraine,Jumatano asubuhi, Agosti 16, 2023.AP.
Ghala iliyoharibiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Russia inaonekana kwenye bandari ya Danube karibu na Odessa, Ukraine,Jumatano asubuhi, Agosti 16, 2023.AP.

Gavana wa Odesa Oleh Kiper alisema kwenye Telegram shambulio hilo liliharibu ghala na vifaa vya kuhifadhia nafaka

Maafisa wa Ukraine walisema Jumatano kwamba Russia iliharibu miundo mbinu ya kuhifadhi nafaka katika bandari ya Odesa kusini mwa Ukraine kama sehemu ya shambulio la usiku wa kuamkia jana la ndege isiyo na rubani.

Andriy ndriy Yermak, mkuu wa wafanyakazi wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema kwenye Telegram shambulio hilo lililenga bandari ya Reni kwenye mto Danube.

Gavana wa Odesa Oleh Kiper alisema kwenye Telegram shambulio hilo liliharibu ghala na vifaa vya kuhifadhia nafaka kwenye bandari.

Kiper alisema hakuna vifo vilivyoripotiwa kutokana na shambulio hilo, na kusema kwamba jeshi la anga la Ukraine lilitungua ndege 11 za Russia zisizo na rubani dhidi ya Odesa.

Forum

XS
SM
MD
LG