Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:26

Russia yaripotiwa kushambulia na kuharibu miundombinu ya nafaka Ukraine

Picha iliyotolewa na Kitengo cha Huduma ya Dharura cha Ukraine Agosti 14, 2023, ikionyesha wafanyakazi wa uokoaji wakiendelea kupambana na moto kufuatia shambulizi la usiku liliofanywa na Russia huko Odesa. (Photo by Handout / Ukrainian Emergency Service / AFP)

Maafisa wa Ukraine wamesema Russia wameharibu miundombinu ya nafaka katika bandari kwenye eneo la Odesa kusini mwa ukraine kama sehemu ya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani.

Andriy Yermak mkuu wa wafanyakazi wa rais wa ukraine Volodymir Zelensky amesema kwa njia ya telegram shambulizi lililenga bandari ya Reni katika mto Denube.

Video zilizochukuliwa kutoka upande wa Romania kwenye mto huo zimeonyesha milipuko mikubwa , wakati milio ya risasi ikisikika katika video hizo.

Maafisa wa ukraine wanasema ndege zisizokuwa na rubani zimelenga bandari mbili ambazo zilikuwa zinahitaji ghala za nafaka.

Bandari kwenye mto Denube ni mojawapo na maeneo muhimu ya usafirishaji nje wa nafaka za ukraine ambazo zimehifadhiwa katika magunia na halafu kusafirishwa kwenda bandari ya black sena huko costanta.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema leo mifumo ya ulinzi wa anga imeharibu ndege tatu zisizokuwa na rubani za ukraine katika mkoa wa kaluga.

Forum

XS
SM
MD
LG