Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:13

Ukraine: Droni za Russia zashambulia ghala za bandarini katika mkoa wa Odesa


Picha iliyotolewa na Huduma za Dharura za Ukraine Agosti 2, 2023, zinaonyesha jengo lililoharibiwa na droni za Russia katika bandari ya Ukraine
Picha iliyotolewa na Huduma za Dharura za Ukraine Agosti 2, 2023, zinaonyesha jengo lililoharibiwa na droni za Russia katika bandari ya Ukraine

Maafisa wa Ukraine walisema Jumatano kuwa droni za Russia zimeshambulia ghala za bandarini katika mkoa wa Odesa huko Kusini mwa Ukraine, na huku droni zilizotumwa na Russia pia zikilenga mji mkuu wa Ukraine.

Jeshi la Ukraine lilisema kuwa shambulizi la Russia liliharibu mashine ya kubeba nafaka na kusababisha moto katika kiwanda na ghala za bandarini huko Izmail.

Oleh Kiper, gavana wa mkoa wa Odesa, alisema kupitia ujumbe wa Telegram kuwa shambulizi la Russia lilileta uharibifu lakini hapakuna na ripoti zozote za majeruhi.

“Magaidi wa Russia kwa mara nyingine tena wameshambulia bandari kadhaa, nafaka, usalama wa chakula duniani,” alisema Kiper.

Eneo hilo liko kuvuka Mto Danube kutoka Romania, limekuwa ni muhimu katika njia mbadala kwa Ukraine kusafirisha nafaka zake tangu Russia ilipojitoa katika Makubaliano ya Usafirishaji Nafaka ya Black Sea mwezi uliopita.

Tangu kuondoka katika makubaliano hayo, Russia imeendelea mara kwa mara kushambulia miundombinu ya nafaka ya Ukraine katika mkoa wa Odesa.

Uturuki na Umoja wa Mataifa walisaidia kusimamia mkataba huo ulioruhusu upitishaji salama wa nafaka ya Ukraine inayosafirishwa kupitia bahari ya Black Sea.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG