Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:37

Russia yaeleza umuhimu wa kuuteka mji wa Bakhmut, Ukraine yaahidi kuendeleza mapambano


Sergei Shoigu
Sergei Shoigu

Waziri wa Ulinzi wa Russia alisema Jumanne kuwa kuuteka mji wa mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut ilikuwa muhimu kwa kuanzisha operesheni ya mashambulizi ya kina katika mkoa huo, wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiahidi kuendeleza mapambano kwa ajili ya  Bakhmut.

Mkuu wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu ameutaja mji wa Bakhmut kuwa ni kituo muhimu cha kujihami kwa majeshi ya Ukraine wakati akizungumza na maafisa wa jeshi na kusema kutekwa kwake kutayaruhusu majeshi ya Russia kuingia “ndani zaidi katika ngome za ulinzi za Ukraine.”

Katika hotuba yake ya Jumatatu usiku, Zelenskyy alisema makamanda wake wa kijeshi kwa kauli moja wameunga mkono kutoondoka Bakhmut, ambayo imekuwa ni eneo la mapambano makali kwa miezi kadhaa.

“Nimemwambia kamanda mkuu kutafuta vikosi vinavyofaa kuwasaidia wale walioko Bakhmut,” Zelenskyy alisema. Hakuna sehemu yoyote ya Ukraine ambayo mtu anaweza kusema inaweza kutelekezwa. Na hakuna handaki lolote nchini Ukraine ambako ukakamavu na ushujaa wa wapiganaji wetu unaweza kupuuzwa.”

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Jumatatu ikiwa wanajeshi wa Russia watafanikiwa kukamata udhibiti wa mji wa mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut, hilo halitawakilisha mabadiliko makubwa katika mzozo huo.

"Nadhani hiyo itakuwa ni kama thamani ya mfano kuliko ilivyo thamani ya kimkakati na kiutendaji," Austin aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Jordan.

Austin amesema Jumatatu kuwa hauoni uamuzi wa Ukraine wa kuwarejesha wanajeshi wake magharibi mwa mji huo kama pigo la kimkakati kwa Ukraine.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters

XS
SM
MD
LG