Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema katika taarifa yake kupitia mtandao wa kutuma ujumbe wa Telegram kwamba Sergei Shoigu "alikagua kituo cha Kijeshi cha moja ya vikosi vya Russia katika eneo lililo karibu na Kusini mwa Donetsk."
Katika video iliyotolewa Jumamosi, waziri wa ulinzi alionekana akikabidhi nishani kwa vikosi vya jeshi la Russia.
Shoigu amekosolewa kwa Russia kutofanya vyema katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi kwamba "mapigano makali" yanaendelea ndani na karibu na mji wa Bakhmut, jimbo la Donbus..
Ukraine inasema jiji hilo lina thamani ndogo ya kimkakati lakini inasema kushindwa katika eneo hilo kunaweza kuamua mkondo wa vita hivyo.
Taarifa ya kijasusi ya Uingereza kwenye Twitter ilisema Bakhmut inaweza kushambuliwa na Russia kutoka pande tatu, lakini Ukraine inaendela kutuma vikosi vyake huko , kuimarish ulinzi.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya Marekani kutangaza msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine ambao ni jumla ya dola milioni 400.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisema Ijumaa kwamba usaidizi huo uta jumuisha silaha zaidi, ambazo alisema, Ukraine inazitumia ipasavyo kujilinda, pamoja na vifaa vingine muhimu.