Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:30

Wanajeshi na mamluki wa Russia wamezingira Bakhmut, Wagner wameagiza wanajeshi wa Ukraine kuondoka


Mchoro wa picha inayoonyesha Bakhmut ambapo wanajeshi wa Russia na kundi la mamluki la Wagner wmezingira
Mchoro wa picha inayoonyesha Bakhmut ambapo wanajeshi wa Russia na kundi la mamluki la Wagner wmezingira

Wanajeshi na mamluki wa Russia wamefunga njia zilizosalia kuingia mji wa Bakhmut nchini Ukriane leo Ijumaa, ikiwa ni ishara ya ushindi mkubwa wa kwanza kwa Russia katika muda wa miezi wa vita hivyo.

Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner amesema kwamba mji wa Bakhmut, ambao umeharibiwa vibaya sana, umezingirwa na njia moja pekee imesalia kwa wanajeshi wa Ukraine.

Wandishi wa shirika la habari la Reuters, walio magharibi mwa mji huo, wamewaona wanajeshi wa Ukraine wakichimba mahandaki kwa ajili ya kujilinda na kwamba kamanda wa Ukraine katika kitengo cha ndege zisizokuwa na rubani katika mji huo amesema kwamba ameamuriwa kuondoa wanajeshi wake.

Ushindi katika mji wa Bakhmut, uliokuwa na jumla ya watu 70,000 kabla ya vita kuanza, utakuwa wa kwanza mkubwa kwa Russia katika vita vyake vya gaharama kubwa sana, baada ya kutuma maelfu ya wanajeshi wa akiba mwaka uliopita.

Russia imesema mafanikio hayo yatatoa fursa nyingine kwa wanajeshi wake kudhibithi eneo Jirani la Donbas, ambalo ni muhimu katika vita hivyo.

Wanajeshi wa Ukraine walidhibiti sehemu kadhaa katika nusu ya mwaka 2022 na wamekuwa wakipigana kurudisha maeneo hayo kwa muda wa miezi mitatu sasa.

Umuhimu wa mji wa Bakhmut

Ukraine imesema kwamba mji huo hauna umuhimu mkubwa lakini hasara kubwa katika mji huo itakayotokea huko inaweza kuathiri namna vita hivyo vinavyoendelea.

Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin, amerekodi video akiwa amevalia sare za kijeshi, alitoa wito kwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuwaamuru wanajeshi wake kuondoka Bakhmut ili kuokoa Maisha yao.

"Huu ni ujumbe kwa Volodymyr Zelensky kwamba wapiganaji wa Wagner wameuzingira mji wa Bakhmut na njia moja tu imesalia. Wanakaribia kuuteka mjia huo,” amesema Prigozhin.

Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kharkiv wanasubiri kufikishiwa vifaru vya kivita ambavyo wamesema kwamba vitapelekea wanajeshi wa Russia kuogopa sana na kubadilisha mkondo wa vita hivyo.

Dereva wa vifaru vya Ukraine, wanavyotumia sasa, amesema kwamba vifaru vyao vinaweza kuharibika wakati wowote.

“Tukiwa na vifaru vipya, tunaweza kupiga hatua kubwa. Vifaru hivi ni vizuri lakini vinaweza kuharibika wakati wowote. Sidahani kama tutakuwa na matatizo makubwa tukipata vifaru vipya. Tutafanya kazi yetu vyema zaidi.”

Marekani imesisitiza kwamba itaendelea kusaidia Ukraine

Msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa nchini Marekani John Kirby, amesema kwamba mazungumzo ya ngazi ya juu ya moja kwa moja tangu Russia ilipoivamia Ukraine, kati ya Marekani na Russia, yalikuwa ya muda mfupi sana lakini ujumbe muhimu uliwasilishwa.

Kirby amesema kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, alitumia fursa iliyopatikana kuwasilisha hoja tatu muhimu.

“Ulikuwa mkutano wa pembeni. Walikuwa katika chumba kimoja wakati wa mkutano wa G20 mjini New Delhi na waziri Blinken alichukua fursa hiyo kuwasilisha hoja muhimu. Moja ni kwamba hatutaki Russia kusitisha makubaliano ya matumizi ya silaha za nyuklia ya START kwa sababu makubaliano hayo yanazifanya nchi zetu mbili kuwa salama. Pili ni kwamba tunataka Paul Whelan arejeshwe. Tuliwasilisha mapendekezo wanstahili kuyakubali. Na tatu ni kwamba tutaendelea kuisaidia Ukraine.”

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Joe Biden katika katika ikulu ya rais wa Marekani - White house kujadiliana namna ya kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Ujerumani ni mtengenezaji wa vifaru aina ya Leopard na inatarajiwa kuwa muhimu kwa wnajeshi wa Ukraine, vitakapowasili baadaye mwaka huu.

Marekani inatarajiwa kutangaza msaada wa kijeshi wa dola milioni 400 hasa risasi na magari ya kijeshi.

Marekani imetoa kiasi cha dola bilioni 32 kama msaada kwa silaha kwa Ukriane tangu vita hivyo vilipoanza.

XS
SM
MD
LG