Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:15

Mwanasheria Mkuu akubaliana na Baraza la Seneti kuliweka kundi la Wagner katika orodha ya taasisi za kigaidi za kigeni


Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland
Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland anasema “hatopinga” kuliweka kundi la mamluki la Wagner la Russia katika orodha ya taasisi za kigaidi za kigeni, akimwita muanzilishi wake, Yevgeny Prigozhin, “mhalifu wa kivita.”

Katika ushahidi mbele ya Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti Jumatano, Garland aliulizwa na Seneta Mrepublikan Lindsey Graham, muungaji mkono mkuu wa Ukraine, iwapo anakubaliana kuwa kikundi cha Wagner “kiorodheshwe katika orodha ya taasisi ya kigaidi za kigeni kwa mujibu wa sheria za Marekani.”

“Nafikiri kuwa wao ni taasisi ambayo inatenda uhalifu wa kivita, taasisi inayoihujumu Marekani,” Garland alisema, akieleza kuwa utaratibu wa kuiorodhesha unafanywa na Wizara ya Mambo ya Nje.

Graham, pamoja na kundi la maseneta wa pande zote, anadhamini sheria ambayo itamuelekeza waziri wa mambo ya nje kuliweka kundi la Wagner kama taasisi ya kigeni ya kigaidi.

Akishinikizwa na Graham iwapo yeye “atapinga kuwekwa kwa kundi hilo katika orodha ya taasisi za kigeni za kigaidi,” Garland alisema, “sipingi hilo, lakini hatimaye nitalipeleka Wizara ya Mambo ya Nje.”

Japokuwa Wizara ya Sheria haihusiki husika moja kwa moja katika kuorodhesha makundi ya kigeni ya kigaidi, matamshi ya Garland yanaonyesha kukubaliana na hatma ya Wagner kuorodheshwa.

Kabla ya kuliorodhesha kundi, Waziri wa Mambo ya Nje anatakiwa kushauriana na mwanasheria mkuu na waziri wa fedha.

XS
SM
MD
LG