Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:40
VOA Direct Packages

Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy akutana na viongozi wa EU mjini Kyiv


Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy akiwa na balozi wa EU nchini mwake Matti Maasikas kwenye picha ya maktaba.
Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy akiwa na balozi wa EU nchini mwake Matti Maasikas kwenye picha ya maktaba.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy Ijumaa amekutana na viongozi wa EU mjini Kyiv akitarajia kuharakisha mkakati wa taifa lake kujiunga kwenye umoja huo, pamoja na kushinikiza vikwazo zaidi dhidi ya Russia.

Hata hivyo wachambuzi wanasema kwamba huenda hilo lisifanyike kwa haraka licha ya haja kubwa iliyopo ili kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini mwake. Ingawa EU imekuwa ikitoa msaada wake kwa Ukraine, bado haijaonyesha azma ya kuharakisha kuipokea kwa haraka kwenye umoja huo.

Kabla ya kikao cha Ijumaa, Zelenskyy alikutana na mkuu wa EU Ursula von der Leyen Alhamisi wakati akimshukuru pamoja na wenzake kutoka EU, kwa msaada wao katika kulinda taifa lake pamoja na watu wake. Wakati huo huo wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba kundi la Wagner la Russia limepunguza viwango vya kuwashirikisha wafungwa kwenye mapigano.

Ripoti zimeongeza kusema kwamba idara ya jela ya Russia imeshuhudia kupungua kwa wafungwa wanaojiunga kwenye vita hadi 6,000 pekee tangu Novemba mwaka uliopita. Licha ya viongozi wa EU kuwepo nchini Ukraine, Russia imeendelea kufanya mashambulizi kwenye mji wa mashariki wa Kramatosk jana Alhamisi.

XS
SM
MD
LG